Hapo ni Nanyumbu, Mtwara
Hivi Mtwara na Lindi si Tanzania ama?
Katika sehemu mbalimbali nchini unakotumika usafiri wa pikipiki almaarufu bodaboda usalama wa abiria si ishu sana kwani ni dereva tu anayetakiwa kuvaa kofia.
Katika mkoa wa Lindi na Mtwara kofia kwa mteja ni lazima…tembea wilaya zote za mikoa hiyo utajionea. Ukipanda tu anakushikisha anakwambia ‘vaa kofia kwa kuwa tukikamatwa utatozwa sh 40,000 kama faini’. Kama hana kofia ya abiria mkikutwa analipa na wewe unalipa kwa kukubali kupanda bodaboda isokuwa na kofia.
Changamoto huko ni kuwa KOFIA hizo zinazovaliwa na kila mtu, kiafya inakaaje hiyo?